
Gustato Petro amemrejesha nyumbani balozi wa Colombia nchini Ecuador, akimtaka arudi Bogotá “mara moja,” kufuatia uamuzi wa Quito wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Colombia kwa 100%.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchi hizo mbili zimekuwa zikishiriki katika vita vya kibiashara kwa miezi kadhaa, vilivyoanzishwa na Quito, ambayo inadai imelazimika kuongeza matumizi yake ya ulinzi ili kulinda mpaka wao wa pamoja.
Ecuador imemrejesha balozi wake nchini Colombia siku ya Jumatano, Aprili 8, baada ya Rais wa Colombia Gustavo Petro kumwita makamu wa rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas, anayezuiliwa kwa ufisadi, “mfungwa wa kisiasa.”
Kurejeshwa kwa balozi huyo kwa ajili ya mashauriano kunakuja wakati wa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, wakati Quito ilipoishutumu Bogota kwa kushindwa kupambana na uhalifu katika mpaka wao wa pamoja. Colombia pia ilisitisha mauzo ya umeme kwa jirani yake.
Mvutano uliongezeka zaidi wakati Colombia, mnamo mwezi Machi, iligundua bomu la Ecuador ambalo halikulipuka katika eneo lake, kufuatia shambulio la bomu la kijeshi upande wa Ecuador.
Ecuador, kwa usaidizi wa Marekani, inafanya kampeni ya mashambulizi ya anga dhidi ya biashara ya dawa za kulevya ndani ya mipaka yake, ambapo 70% ya kokeini kutoka Colombia na Peru, wazalishaji wakuu duniani, hupitiswa.