
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na Kim Jong-un huko Korea Kaskazini siku ya Ijumaa, Aprili 10. Mkutano huu unaonyesha uhusiano kati ya washirika hao wawili wa kihistoria ulioanza mwezi Septemba. Korea Kaskazini, iliyohusika waziwazi katika vita vya Ukraine pamoja na Moscow, ilikuwa imeweka kipaumbele uhusiano wake na Urusi kwa gharama ya China. Lakini sasa, Beijing na Pyongyang zinasema zinataka kuratibu masuala ya kimataifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kufanya kazi pamoja,” “kuwa na muonekano mpya na wa kisasa katika urafiki wa kijadi”… misemo ya kusisimua ya Shirika la Habari la Xinhua inaonyesha matarajio ya pamoja ya nchi hizo mbili.
Ziara ya Wang Yi inafuatia mkutano wa kilele kati ya Xi Jinping na Kim Jong-un mnamo mwezi Septemba na ziara ya Waziri Mkuu wa China nchini Korea Kaskazini mnamo mwezi Oktoba. Lakini wakati huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa China anaenda mbali zaidi. Alisifu “mafanikio” ya nchi hiyo, licha ya juhudi za Marekani za kuitenga na kuikandamiza.
Rais wa Marekai Donald Trump anatarajiwa mjini Beijing katikati ya Mei, na uvumi umeenea kuhusu mkutano mpya kati ya bilionea huyo na Kim Jong-un.
Wang Yi na kiongozi wa Korea Kaskazini wameeleza nia yao ya kuratibu masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.
“Kutokana na hali ya kimataifa iliyojaa mabadiliko na machafuko yanayotegemeana, China na Korea Kaskazini, katika kulinda kwa uthabiti uhuru wao, usalama, na maslahi ya maendeleo, zinapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, na kuchangia kikamilifu katika kutetea maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na kulinda amani na maendeleo ya dunia,” ameandika msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian kwenye X.
Beijing inasalia kuwa mshirika mkuu wa kiuchumi wa Korea Kaskazini, na nchi hizo mbili zina maslahi mengi ya pamoja, lakini wakati mwingine zina maono tofauti.
Katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya China na Japan, Pyongyang imeendelea kuonekana kuunga mkono Beijing, huku ikiiacha Washington kwa kiasi fulani. Wakati huo huo, China imekaribia Seoul, iliyotajwa rasmi kama “adui mkubwa wa Korea Kaskazini.”