
Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance yuko njiani kuelekea Pakistan Jumamosi, ambapo mazungumzo kati ya Marekani na Iran yatafanyika huku kukiwa na hali ya kutoaminiana. Mazungumzo hayo yanalenga kukomesha vita Mashariki ya Kati baada ya wiki sita za migogoro.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya kuondoka siku ya Ijumaa, J.D. Vance anatarajiwa kutua asubuhi huko Islamadad – chini ya ulinzi mkali – akiongoza ujumbe wa Marekani, akiambatana na mjumbe maalum Steve Witkoff na Jared Kushner, mkwe wa Donald Trump.
Akiongoza ujumbe wa watu zaidi ya 70, Spika wa Bunge la Iran, mwenye ushawishi mkubwa, Mohammad Bagher Ghalibaf, aliwasili Pakistan siku ya Ijumaa jioni.
Makamu wa rais wa Marekani J.D. Vance hakuwa anataka vita nchini Iran, na sasa aepewa jukumu la kuvimaliza.