Nchini Hungary, Waziri Mkuu Viktor Orban, amekubali kushindwa, kwenye uchaguzi wa wabunge baada ya chama cha upinzani cha Tisza kinachoongozwa na Peter Magyar, kupata ushindi mkubwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ushindi wa chama cha Tisza, ambacho kimeshinda kwa asilimia 97.35 ya kura, unamaanisha kuwa Peter Magyar anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya.
Kuanguka kwa chama cha Fidesz, kunamaliza uongozi wa miaka 16 ya Viktor Orban, ambaye chama chake kimeibuka na asilimia 37.8.
Akikubali kushindwa, Orban amesema, matokeo hayo ni maumivu makubwa kwake na chama chake, lakini ameheshimu maamuzi ya raia wa Hungary.
Umoja wa Ulaya umewapongeza wananchi wa Hungary kwa kumchagua Magyar, wakisema wamechagua Ulaya.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amempigia simi na kumpongeza Magyar kwa ushindi na kusema, inakaribisha ushindi huo wa kidemokrasia.
Marekani, haijazungumzia matokeo hayo, baada ya Orban ambaye alikuwa anaungwa mkono na rais Donald Trump kushindwa kwenye uchaguzi huo. Orban alikuwa kuwa mshirika wa karibu wa Rais Vladmir Putin wa Urusi.