Dar es Salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Look Basila Mwanukuzi amekabidhi umiliki wa uandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania kwa kampuni ya Lamata Village Entertainment inayomilikiwa mwongoza filamu nchini Leah Mwendamseke ‘Lamata’.

Mkurugenzi wa kampuni ya Look Basila Mwanukuzi akifanya makabidhiano ya umiliki wa uandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania kwa mkurugenzi wa kampuni ya Lamata Village Entertainment, Leah Mwendamseke leo Jumanne Aprili 14, 2026 jijini Dar es Salaam.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 14,2026 ambapo yatamruhusu Lamata kuendesha shughuli za shindano hilo la kuwapata warembo nchini.

“Tulibeba slogani ya urembo ni heshima na kweli tumeheshimisha Tanzania. Lakini ni bado jukwaa la kutoa warembo wengine wataofanya mambo makubwa zaidi. Na leo historia inaenda kuwekwa nchini Tanzania. Hili jukumu nililichukua muda mrefu. 

Marehemu Hashim Lundenga aliyesimamia mashindao hayo mwaka 1994 hadi 2018 

“Na sio tu biashara nimewekeza natakiwa nijue namuachia nani, walijitokeza hadi Waturuki wenye fedha zao wanataka brand ya Miss Tanzania. Lakini siwezi kufanya hivyo kwa sababu nina deni. Ilinichukua muda mimi namatumaini makubwa sana na mwanzo wa siku hii ya leo, Lamata historia yake inafahamika mimi pia sina shaka tunatakiwa kumsapoti na kusapoti mabinti zetu ,” amesema Mwanukuzi wakati wa kukabidhi kijiti hicho

Kabla ya kijiti cha shindano hilo kukabidhiwa kwa Lamata. Juni 25,2025 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilifuta kibali cha Kampuni ya The Look kuendesha shindano la Miss Tanzania.

Kufuatia taarifa ya kufutiwa kibali Baraza hilo lilieleza kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza maagizo halali ya Baraza licha ya kupewa maelekezo kwa nyakati tofauti kupitia barua yenye kumbukumbu namba AE/90/90/03/16 ya Aprili 15, 2025, na AE.90/90/03/19 ya Mei 09, 2025.

“Kushindwa kuhuisha kibali cha kufanya kazi za sanaa kwa zaidi ya miezi sita bila sababu ya msingi, kinyume na Kanuni ya 39(g) ya Kanuni za BASATA za mwaka 2018. Kukaidi agizo la Baraza kwa kutowasilisha nyaraka muhimu kama nakala ya cheti/leseni ya kushiriki shindano la Dunia, kinyume na Kanuni za 39(f), 37(2)(a) na 36(2),” taarifa ya Baraza ilieleza 

Taarifa hiyo iliendelea kueleza “Kushindwa kuandaa shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2023/2024 na kutokuwasilisha mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya dunia kwa mwaka 2024/2025, bila kutoa sababu za msingi, jambo linalokiuka Kanuni ya 39(i).

Mkurugenzi wa kampuni ya Look Basila Mwanukuzi aliyemkabidhi Lamata shindano la Miss Tanzania

“Kwa mujibu wa Kanuni ya 40(2) ya Kanuni za BASATA za mwaka 2018, kampuni hiyo imeondolewa sifa ya kuendelea na shughuli hiyo,”

Ikumbukwe awali mashindano hayo yalikuwa yanasimamia na marehemu Hashim Lundenga tangu mwaka 1994 hadi 2018 ambapo alimuachia kijiti Basila Mwanukuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *