
Rais wa China Xi Jinping amempokea Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez leo Jumanne, Aprili 14, kwa ziara rasmi ya siku tatu, shirika la habari la serikali Xinhua limeripoti.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Pedro Sanchez ameanza ziara rasmi ya siku tatu nchini China siku ya Jumatatu yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara, wakati ambapo mvutano uliongezeka katika uhusiano kati ya Madrid na Washington.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, siku ya Jumatatu, alianza ziara yake ya nne nchini China tangua miaka mingi iliyopita, akisisitiza azimio lake la kuongoza njia huru ambayo imemkasirisha Rais wa Marekani Donald Trump.
Uhspania imekuwa mojawapo ya watetezi wakuu wa Ulaya wa kupanua biashara na kuichukulia China kama mshirika wa kimkakati badala ya mpinzani wa kiuchumi na kisiasa kulingana na Rais wa Marekani Trump.
Ziara hiyo inaangazia azimio la Sanchez la kutojilinganisha na Trump – ambaye ameikosoa vikali Uhispania kwa kukataa haki za kutua kwa vikosi vya Marekani katika vita na Iran na kwa matumizi yake ya chini ya ulinzi – na kutishia kuwaadhibu washirika wa kijeshi wa NATO wasio na ushirikiano.
Mbinu ya Sanchez inapendwa na wapiga kura, lakini imewashtua viongozi wa makampuni na wanasiasa wa upinzani ambao wana fofu kwamba mvutano na utawala wa Marekani unaweza kusababisha madhara kwa Uhispania.
Chanzo cha serikali ambacho hakikuruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari kilisema mkutano wa Jumanne na Rais Xi Jinping utazingatia siasa za kijiografia, na kwamba Uhispania inaona China kama nguvu ya kuleta utulivu.
Hata hivyo, Ramon Gascon Alonso, mratibu wa Asia-Pasifiki wa Klabu ya Wauzaji na Wawekezaji ya Uhispania, alisema lengo hili linaweza kuathiri zaidi biashara inayolemewa na ushuru wa Trump kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Umoja wa Ulaya, na “kufanya hali yetu ambayo tayari ni hatari kuwa mbaya zaidi”.