
Wawakilishi wa Lebanon na Israel wanakutana Washington leo Jumanne, Aprili 14, chini ya upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, kwa ajili ya mazungumzo ya awali ya amani ya moja kwa moja. Lakini matarajio ya makubaliano yanaonekana kuwa madogo. Hata kabla ya mkutano huo, mkuu wa Hezbollah inayounga mkono Iran, Naim Qassem, siku ya Jumatatu, alitoa wito wa kufutwa kwa mazugumzo hayo, akisema kwamba mazungumzo kama hayo yatakuwa “kujisalimisha tu.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi wa Hezbollah alitoa wito Jumatatu wa kufutwa kwa mkutano uliopangwa kufanyika Jumanne jijini Washington kati ya Lebanon na Israel, akisema kwamba mazungumzo kama hayo yatakuwa “kujisalimisha tu.”
Lebanon na Israel wamekubaliana kufanya mkutano wa awali leo Jumanne katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Hata hivyo, Israel inahakikisha kwamba hakutakuwa na majadiliano ya kusitisha mapigano na Hezbollah.
Jeshi la Israel latangaza kifo cha mwanajeshi mmoja kusini mwa Lebanon
Jeshi la Israel limetangaza leo Jumanne kifo cha mwanajeshi wake kusini mwa Lebanon, ambapo Israel na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran wamekuwa wakipigana kwa zaidi ya mwezi mmoja.
“Sajenti Meja Ayal Uriel Bianco, mwenye umri wa miaka 30, dereva wa lori la zimamoto, ameuawa akiwa vitani kusini mwa Lebanon,” jeshi la Israel limesema katika taarifa.