Katika dunia ya sasa inayokabiliwa na changamoto za uongozi na uwajibikaji, maadili yameendelea kuwa dira muhimu inayowaongoza watumishi wa umma na viongozi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Maadili yanatajwa kuwa msingi imara na nguzo kuu ya kujenga jamii bora, kuimarisha utoaji wa huduma zenye ubora, pamoja na kuchochea maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla.
Akizungumza mkoani Morogoro katika mafunzo ya maadili kwa viongozi wa umma, Katibu na Mtendaji Mkuu mstaafu wa Ofisi ya Rais – Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Methew Kirai, amesema maadili si hiari bali ni hitaji la lazima na msingi wa mafanikio kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Kwa upande wake, Katibu Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini, Gerald Mwaitembele, ameeleza umuhimu wa mafunzo hayo akisisitiza kuwa ni msingi usiokwepeka katika kujenga uongozi wenye uwajibikaji na uadilifu.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza Ujuzi na maarifa mapya katika utelekelezaji wao wa kazi huku akieleza kuwa wao watakiwa mabalozi wazuri kwa wengine katika kuwapatia ujuzi huo kuhusu umuhimu wa maadili na uadilifu sehem za kazi.
Mafunzo hayo yanatajwa kuwa nyenzo muhimu ya kuwawezesha viongozi wa umma kuzingatia misingi ya maadili katika utendaji wao wa kila siku, jambo linalotarajiwa kuimarisha imani ya wananchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
(Feed generated with FetchRSS)