Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongo Fleva Marioo amtaka msanii wa Kenya Nadia Mukami kutolea ufafanuzi kauli yake iliyodai kusumbuliwa alipokuwa akifanya kolabo na moja ya wasanii wa Bongo Fleva.

Hayo yamekuja baada ya marioo kudai jina lake limekuwa likihusishwa kauli hiyo ya msanii huyo wa Kenya. Huku akikanusha madai hayo na kusema upande wake alifanya kazi na Nadia kwa ushirikiano bila changamoto yoyote.

“Nadia kuja useme nani alikusumbua tafadhari, maana naona huu mzigo unanielemea mimi wakati nilijitoa 100% kwa project yako 2020,”ameeleza Marioo

Ikumbukwe Nadia alisimulia hayo katika moja ya mahojiano bila kutaja jina la msanii huku akisema  kolabo hiyo  ilimtesa . 

“Kuna msanii alitutese ila tulisameheana sio projekti ya kitambo. Nilitumia milioni nyingi sana kwa ajili ya hiyo projekti ilikua timu ya watu sita. Tumeenda Tanzania kwa gari tulifika usiku tulale tushoot video asubuhi tumalize kwa sababu nilikuwa na show.

“Unaona hizo gharama mavazi, chakula, mafuta, kukodi gari. Nikapigia msanii akasema ameenda kwenye show atakuja asubuhi iliyofuata tukaanza kupigia simu msanii na meneja hawakupokea. Tulitakiwa tuanze saa tatu asubuhi msanii alifika 7PM.

“Siku nzima tulikaa tu kumsubiri, nililia meneja alivyopokea simu akasema msanii amechoka anapumzika kidogo, alivyofika hakunisalimia akaenda akabadili nguo ndio akaja nikamwambia ni sawa tushoot,”alieleza Nadia katika mahojiano yake

Nadia na Marioo wamefanya pamoja wimbo uitwao ‘Jipe’ uliotoka miaka sita iliyopita. Hadi sasa kwenye mtandao wa YouTube umetazamwa zaidi ya mara milioni tano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *