
Tukio hili la kusikitisha limesababisha msukosuko mjini Kinshasa. Mjasiriamali ambaye alikuwa bado kijana alipatikana amefariki, akipigwa risasi hadi kufa asubuhi na mapema ya Aprili 10. Vally Amisi, meneja wa klabu ya mpira wa miguu katika mji mkuu, alikuwa mtu maarufu katika ulimwengu wa michezo wa Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi
Hapo awali, mamlaka zilipendelea nadharia ya utekaji nyara na genge lenye silaha, lakini maendeleo mapya yamesababisha uchunguzi kushuku kuhusika kwa mtu wa karibu naye. Tangu kutangazwa kwa kifo cha kiongozi huyo wa michezo, rambirambi kwa kijana huyo zimefurika kwenye mitandao ya kijamii.
Vally Amisi, mkazi wa Afrika Kusini, alikuwa Kinshasa kikazi alipouawa na mwili wake kutelekezwa kwenye uchochoro huko Gombe, kituo cha utawala na uchumi cha mji mkuu wa DRC. Nadharia ya utekaji nyara wa genge lenye silaha ilifutiliwa mbali haraka.
Siku ya Jumapili jioni, siku mbili baada ya ugunduzi huo wa kutisha, notisi ya utafutaji ilitolewa na mamlaka. Ilimlenga mshukiwa ambaye, kulingana na wachunguzi, alionekana katika video kadhaa za kamera za usalama (CCTV) pamoja na mwathiriwa, ambaye alikuwa karibu naye. Katika picha hizi, ambazo zilivuja kwenye mitandao ya kijamii, Vally Amisi anaonekana akiingia kwenye nyumba na mtu ambaye sasa anachukuliwa kuwa mshukiwa mkuu.
Saa chache baadaye, mshukiwa anaonekana akiondoka kwenye nyumba hiyo peke yake akienda kuzuia kamera ya usalama kwenye korido. Kisha, video ya mwisho inaonyesha mwanamume huyo akiwa kwenye lifti akiwa na kile kinachoonekana kama mwili wa mtu aliyefariki miguuni pake. Mshukiwa anaripotiwa bado hajakamatwa, lakini Wizara ya Sheria inabainisha kwamba kila kitu kinafanywa ili kuangazia mauaji haya na kwamba watu kadhaa tayari wamekatamwa.