Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa kumi na nne, leo anatarajiwa kuzuru Bamenda, eneo ambalo limeendelea kukabiliwa na utovu wa usalama kwa miaka kadhaa sasa, kati ya kundi linalotaka eneo hilo ambalo wakaazi wake wanaozungumza Kiingereza kujitenga na kujitawala.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ziara hii ni muhimu kwa wakaazi wa Bamenda, wanaoamini kuwa ujio wa Papa huenda ukasaidia kutatua mzozo huo ambao kwa zaidi ya miaka 10, maellfu ya watu wamepoteza maisha na wengine Milioni moja, kuyakimbia makaazi yao.
Utekaji umeshamishiri katika eneo hilo, huku shule zikifungwa kwa sababu za kiusalama. Akiwa Bamenda, Papa Leo wa kumi na nne, atakuwa na kikao kuhusu amani na baadaye kuongoza misa kwenye viwanja vya uwanja wa ndege.
Hii ni ziara ya nne, kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kuwahi kutembelea taifa hilo la Afrika ya Kati, mara ya mwisho ikiwa ni ziara ya Papa Benedict wa kumi na sita mwaka 2009.
Akimkaribisha Papa Leo, siku ya Jumatano, Rais Paul Biya kiongozi mkongwe duniani mwenye umri wa miaka 93, alitoa wito wa amani akitoa wito kwa kundi hilo linalopigana kuweka silaha chini.