Maelezo ya Serikali ya Burundi, kuhusu mazingira ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa mawasiliano na Habari, Gabby Bugaga, yameibua maswali zaidi baada ya mwili wake kukutwa kwenye gari, tukio ambalo serikali imesema kifo chake kilisababishwa na ajali.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Licha ya serikali kutoa taarifa rasmi na kueleza kuwa kifo cha waziri huyo kimetokana na “ajali ya ghafla” sauti zimekuwa zikiongezeka zikitaka uchunguzi huru ufanyike, ikiwa ni pamoja na ule kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu kama King Umurundi Freddom.

Mwili wa Gabby Bugaga ulipatikana kilomita 10 kaskazini mwa Bujumbura, katika shamba la mitende la Kivoga, kwenye barabara ambayo haitumiki sana usiku.

Katika picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitishwa kuwa halisi, Waziri huyo anaonekana amekufa, akiwa amevaa fulana akiwa nusu amelala kwenye kiti cha mbele. Jeraha kubwa linaonekana kichwani, huku gari lake likionekana kuwa salama.

Kuhusu gari, hilo jeusi la kubeba mizigo, kuna uharibifu unaoonekana nyuma na kulia. Taa za mbele zimeharibika, lakini bampa liko salama.

Maswali mengi yameibuka kwenye mitandao ya kijamii hasa kuhusu uwepo wa Waziri katika barabara hii wakati wa usiku sana… na hasa uwepo wake pekee yake bila dereva au walinzi.

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka wa 2025. Gaby Bugaga alianza kazi yake kama mwandishi wa habari kwenye kituo cha redio na televisheni ya kitaifa. Tarehe ya mazishi yake bado haijabainishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *