Dar es Salaam. Wakati dunia ikiwa katika mapambano ya kukabiliana na bei za mafuta, wanaotumia malori katika shughuli zao sasa wanaenda kupata ahueni baada ya kutarajiwa kuletwa kwa magari hayo nchini yayotumia gesi asilia.
Mgogoro wa mafuta umekuwa mkali kutokana na vita inayoendelea kati ya Marekani na Iran.
Mgogoro huo umeathiri uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ghafi duniani, hasa baada ya kufungwa kwa Mlango wa Hormuz, ambao hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yote yanayosafirishwa duniani.
Vilevile, kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kuyasafisha kumeigusa moja kwa moja Tanzania ambayo inaagiza mafuta kwa kiasi kikubwa, jambo linalotajwa kuongeza gharama za usafirishaji kutokana na kukosekana kwa meli za kuyasafirisha.
Baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa kampuni ya Saturn, wakiwemo mafundi na wahandisi, ambao wamefundishwa na kampuni hiyo kuhusu masuala ya uunganishaji wa malori mazito na magari.
Akizungumzia hatua hiyo ya kuleta malori yanayotumia gesi, Afisa Mkuu wa Uendeshai wa Saturn Corporation, Mehul Sachdev, amesema kuwa uamuzi huo wa kimkakati umezingatia hali halisi ya uendeshaji.
Lakini pia ni latika kampuni kupanua wigo wa bidhaa zake ili kukidhi mahitaji na shinikizo la ongezeko la gharama katika sekta ya usafiri.
“CNG ni mbadala unaotekelezeka kwa dizeli, unaotoa faida za kupunguza gharama pamoja na kulinda mazingira.
“Hivyo tunaiona kama nyongeza ya vitendo katika huduma zetu, inayowapa watu wetu uhuru zaidi katika kusimamia gharama za mafuta huku tukijibu pia ongezeko la mahitaji ya nishati safi,” amesema Sachdev.
Amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho mwaka 2024, kimeonyesha ukuaji thabiti katika uwezo wa uzalishaj na upanuzi wa soko, na kujipambanua kama mdau muhimu katika sekta ya uunganishaji magari nchini.
Kampuni hiyo ni muunganishaji na msambazaji rasmi wa Sinotruk kutoka China, ikiwa na kiwanda chake kikuu Kigamboni, Dar es Salaam.
Uongozi wa kampuni unaeleza kuwa kuanzishwa kwa teknoloyia ya CNG ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kumarisha uzalishaji wa ndani huku ikiendana na mwelekeo mpya wa nishati,
“Tunaendelea kujenga operesheni inayokwenda sambamba na mwelekeo wa soko kwa kuunganisha teknolojia ya CNG katika mstari wetu wa uzalishaji kunatuwezesha kuwa mbele ya mahitaji ya soko huku tukiendelea kutoa suluhisho za usafiri zilizo imara na zenye gharama nafuu,’ aliongeza Ofisa huyo.
Kwa sasa, kiwanda cha Kigamboni kimethibitisha kama mojawapo ya viwanda vikubwa na vya kisasa zaidi vya kuunganisha malori katika ukanda huu kikiweka viwango vya juu katika sekta ya viwanda.
Kina uwezo wa kuzalisha hadi malori 22 kwa siku, sawa na takriban malor 536 kwa mwezi, hali inayoonyesha ukubwa na ufanisi wa opereshens zake .
Kwa uwezo mkubwa wa kuunganisha na kubinafsisha malori ya uzito mkubwa, amesema kampuni inaendelea kusaidia sekta muhimu za uchumi, ikiwemo ujenzi, uchimbaji madini, usafirishaji, kilimo na maendeleo ya miundombinu, ambazo zote ni nguzo muhimu za ukuaji wa Tanzania.
Sachdev ameongeza kuwa kadri mahitaji yanavyoendelea kuongezeka, Saturn inapanga kuongeza uzalishaji hatua kwa hatua, lengo likiwa ni kufikia jumla ya magari 10,000 ifikapo mwaka 2027.
“Uanzishaji wa malori yanayotumia CNG unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya upanuzi huu, huku uzalishaji ukiongezeka kulingana na mahitaji ya soko na maendeleo ya miundombinu.
Hayo magari yanatarajiwa kuketwa mwishoni mwa mwaka huu, naomba niongezee hapo.