Mwanaharakati wa Panafricanist, mshawishi, na mwandishi Kemi Seba anatarajiwa kufika mahakamani nchini Afrika Kusini mnamo Aprili 20. Alikamatwa wiki iliyopita mjini Pretoria, na kufuatia hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa na Benin kufuatia kuunga mkono jaribio la mapinduzi mwezi Desemba mwaka uliyopita, kwa sasa yuko kizuizini kabla ya kesi na atafika mahakamani leo Jumatatu pamoja na mmoja wa wanawe na raia mwingine wa Afrika Kusini anayetuhumiwa kumsaidia kufika Zimbabwe.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Johannesburg, Valentin Hugues

Mahakama ya Afrika Kusini itatoa kwanza uamuzi kuhusu suala la uhamiaji haramu. Kemi Seba amekuwa Afrika Kusini kwa takriban miezi mitano. Visa yake iliisha miezi miwili iliyopita, kulingana na wasaidizi wake, na mshawishi huyo alikuwa akijiandaa kuvuka mpaka na kuingia Zimbabwe alipokamatwa.

Lakini zaidi ya suala la uhamiaji, polisi wa Afrika Kusini wanataja operesheni ya siri, iliyofanywa na Interpol, ambayo ilisababisha kukamatwa kwa Kemi Seba. Mshawishi huyo anatafutwa na Benin na anakabiliwa na hati ya kimataifa ya kukamatwa kufuatia kuunga mkono jaribio la mapinduzi la mwezi Desemba mwaka uliyopita.

Ingawa Afrika Kusini inasisitiza kwamba kesi ya kumrejesha nchini  mwake inaendelea, chanzo kilicho karibu na kesi hiyo kinabainisha kwamba kuna uwezekano mdogo sana wa kufanikiwa kutokana na ukosefu wa makubaliano kati ya Benin na Afrika Kusini.

Hii itakuwa kesi ya pili kwa siku leo. Mawakili wa Kemi Seba watajaribu kutatua suala hili la kumrejesha nchini mwake haraka iwezekanavyo na wataomba aachiliwe. Akiachiliwa, Kemi Seba anaweza kuchagua kubaki Afrika Kusini, lakini pia anaweza kusafiri hadi Niger, kwani ana pasipoti ya Nigeria.

Kemi Seba (jina lake halisi ni Stellio Gilles Robert Capo Chichi) ni mwanaharakati wa Panafricanist, mshawishi, na mwandishi mwenye asili ya Benin na Ufaransa, anayefahamika kwa msimamo wake mkali dhidi ya ukoloni mamboleo wa Ufaransa barani Afrika.

Mwanaharakati wa Panafricanism: Kemi Seba ni kuingozi wa shirika lisilo la kiserikali la Urgences Panafricanistes, na anajulikana kama mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mapambano ya uhuru wa kiuchumi na kiutamaduni wa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *