Kampuni ya Doweicare Technology Limited imeupokea rasmi Mwenge wa Uhuru mahsusi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda chao kipya cha bidhaa za taulo za kike cha Softcare kilichopo Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Tukio hilo linaashiria maendeleo makubwa yaliyopatikana na si tu kwa kampuni hiyo, bali pia kwa Taifa zima katika eneo la uimarishaji viwanda vya ndani na uboreshaji ustawi wa jamii.
Mwenge wa Uhuru, ambao ni alama ya kudumu ya umoja, uhuru na maendeleo ya Tanzania, unaendelea na mbio zake za kila mwaka kote nchini.
Kuwasili kwake katika ofisi za Doweicare kumedhihirisha utambuzi wa mchango wa kampuni hiyo katika kukuza viwanda na kuleta athari chanya kwa jamii zinazozunguka shughuli zake.
Katika hafla hiyo, kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Wazo Mwang’onda aliweka jiwe la msingi wa kiwanda hicho cha kisasa.
Ujenzi wa baadhi ya miundombinu bado unaendelea na unatarajiwa kukamilika katika miezi ijayo. Hii inaonyesha dhamira ya muda mrefu ya kampuni katika kuwekeza na kupanua uwezo wake wa uzalishaji.
Muonekano wa jiwe la msingi la kiwanda kipya cha Softcare kilichopo Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani baada ya kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Sherehe hiyo iliwakutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi, wakiwemo viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wanajamii.
Ushiriki wao umeonyesha namna uwekezaji katika viwanda unavyoweza kuwa chachu ya maendeleo jumuishi kwa kuunganisha nguvu za sekta mbalimbali katika kufanikisha malengo ya Taifa.
Kiongozi wa mbio za Mwenge, uongozi wa Doweicare wazungumza
“Kwanza kabisa, ninapenda kuwapongeza viongozi wa mkoa na wilaya kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa rafiki kwa wawekezaji. Huku ni kumuunga mkono kwa dhati Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unastawi na kuleta tija kwa Taifa letu.”
“Nimejionea mwenyewe kazi nzuri inayofanyika katika eneo hili la viwanda. Kiwanda hiki kilichoanza uzalishaji mwezi Desemba mwaka 2025 kimeleta heshima kubwa sana kwa Wilaya ya Kibaha.
Uzalishaji ni mkubwa, na ninaendelea kuwahimiza wawekezaji kuleta mipango mingine zaidi ili kiwanda hiki kizidi kukua na kuleta manufaa zaidi,” alieleza Wang’onda.
Kiongozi huyo alisema ameguswa sana na mchango uliotolewa na kampuni hiyo kwa jamii.
“Kitendo chenu cha kugawa bidhaa hizi 6,000 kwa wanafunzi 1,000 ili kuimarisha mahudhurio yao shuleni na kuwapa kujiamini kwa kipindi cha miezi sita ni cha kuigwa na kinapaswa kupongezwa sana.”
Wanafunzi wa shule za sekondari ambao ni wanufaika wakinyanyua pakiti za taulo za kike za Softcare juu kwa tabasamu walizozipata kutoka kwa uongozi wa Doweicare.
Baada ya kusema hayo, Mwang’onda aliweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho ambacho ni alama ya maendeleo na heshima kwa Taifa letu.
Akiwakaribisha wadau wote katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Doweicare, Han Cheng ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Softcare alisema kuwa uwekezaji huo wa mabilioni ya fedha unaonyesha imani yao kwa Tanzania na azma yetu ya kuunga mkono maendeleo ya viwanda nchini.
“Tungependa kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake thabiti katika kuweka mazingira ya amani, utulivu, na yanayovutia wawekezaji.
Pia, tunawashukuru viongozi wa serikali waliopo hapa leo; kujitolea kwenu kuwatumikia wananchi ndiko kunakofanya maendeleo ya kweli yawezekane,”
“Tunajivunia kuwa Softcare imetambuliwa kama Chapa Bora ya Nepi za Watoto barani Afrika, jambo ambalo ni kielelezo cha jitihada zetu katika ubora na weledi.”
“Kama kampuni, tunaendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania kupitia uzalishaji wa ajira, ulipaji kodi, na uzalishaji wa bidhaa mbadala wa zile zinazoagizwa kutoka nje,” alihitimisha Cheng.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon (wa tatu kulia), Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Doweicare, Han Cheng (wa tatu kushoto) na wanafunzi wa shule za sekondari wanufaika wakiwa katika picha ya pamoja huku wamebeba pakiti za taulo za kike za Softcare.
Naye Meneja Masoko wa Doweicare, Lucia Msami alibainisha kuwa uwekezaji wa Doweicare ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kuendeleza kongani za viwanda zilizotengwa mahsusi kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa ndani.
“Kiwanda hicho kilichopo katika Kongani ya Misugusugu kilianza kujengwa Novemba 2024 na kuanza uzalishaji rasmi Desemba 2025, kikiwa na uwekezaji unaozidi Dola za Marekani milioni 16 (takribani Sh40 bilioni),”alifafanua Lucia na kuongeza:
“Aidha, kiwanda kinazalisha bidhaa mbalimbali za usafi binafsi ikiwemo taulo za watoto, taulo za kike na wipes za watoto, huku kikitoa ajira kwa takribani watu 360, wengi wao wakiwa vijana,” anaeleza na kuongeza.
Lucia alisisitiza kuwa pamoja na uzalishaji, kampuni imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kwa jamii, hususan kupitia sekta ya elimu kwa kusaidia wasichana kupata vifaa vya kujisitiri ili kuimarisha mahudhurio naufaulu wao shuleni.
Ugawaji taulo za kike: Kuimari sha ustawi wa wasichana kupitia hedhi salama
Mbali na uzinduzi wa kiwanda hicho, Doweicare imeonye sha dhamira yake kwa maende leo ya jamii kwa kutoa msaada wa pakiti 6,000 za taulo za kike aina ya Softcare kwa wanafunzi 1,000 wa kike kutoka shule tatu za sekondari zilizo karibu na kiwanda hicho.
Msaada huo utawasaidia wanafunzi hao kwa kipindi cha miezi sita mfululizo. Mpango huo unalenga kuhakikisha wasicha na wanahudhuria masomo yao bila kukatizwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa salama vya kujisitiri wakati wa hedhi.
Kwa miaka mingi, upatikanaji mdogo wa bidhaa nafuu za hedhi umechangia utoro mashuleni kwa wasichana, hali inayodhoofisha maendeleo yao ya kitaaluma na ustawi wao kwa ujumla. Kupitia msaada huu, Doweicare inachangia moja kwa moja kutatua changamoto hiyo kwa kutoa suluhisho linalotakiwa.
Wasichana hivi sasa wataweza kuhudhuria masomo kwa kujiamini, heshima na utulivu wa akili. Aidha, mpango huu unasaidia kuondoa unyanyapaa unaozunguka suala la hedhi huku ukihamasisha matumizi ya njia salama zaidi.
Mpango huu ni sehemu ya mka kati mpana wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) wa kampuni hiyo, unaolenga kuboresha maisha ya jamii inayozunguka mazingira ya kampuni hiyo. Ujumbe muhimu wanaousam baza hapa kwa watu ni kwamba hakuna msichana anayepaswa kulazimika kuchagua kati ya elimu yake na mzunguko wake wa kibaolojia.
Ndani ya kiwanda cha Softcare: Ubunifu na viwango vya juu vya ubora
Kiwanda cha Softcare kinawakilisha hatua kubwa kati ka safari ya Tanzania kuelekea kujenga uchumi wa viwanda unaojitegemea. Wageni waliohu dhuria walipata fursa ya kutem belea kiwanda hicho na kujionea teknolojia ya kisasa inayotumika katika uzalishaji.
Mchakato wa uzalishaji umeboreshwa kwa kutumia mifumo ya kiotomatiki kuanzia uchakataji wa malighafi hadi ufungashaji wa mwisho wa bidhaa hizo, ambapo hakuna usimamizi wa kibinadamu kwenye hatua hiyompaka bidhaa inapokamilika.
Faida iliyopo hapa ni kusaidia kupunguza bidhaa kuchafuka kwa urahisi na kuhakikisha viwango vya juu vya usafi na ubo ra vinakuwepo. Bidhaa zinazozalishwa ni salama, zina uwezo mkubwa wa kunyonya uchafu na zimeundwa kukidhi mahitaji ya watumiaji wa ndani pamoja na viwango vya kimataifa.
Hali hii inaifanya Softcare kuwa chapa yenye ushindani mkubwa katika soko la bidhaa za usafi. Mbali na ubora wa bidhaa, kiwanda hicho tayari kimeanza kuleta manufaa ya kiuchumi kwa kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo na kupunguza utegemezi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi. Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa ndani na kuongeza thamani ya uzalishaji wa ndani.
Kadiri Doweicare inavyoendelea kupanua shughuli zake, mkakati wake wa kuunganisha ukuaji wa biashara na uwajibikaji kwa jamii unaifanya kuwa mfano bora wa maendeleo jumuishi. Kampuni inaonyesha kuwa mafanikio ya biashara yanaweza kwenda sambamba na ustawi wa jamii.
Meneja Masoko wa Doweicare Lucia Msami akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la kiwanda kipya cha Softcare kilichopo Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Kwa ujumla, uwekezaji wa Doweicare hauishii katika uten genezaji wa taulo za kike pekee, bali unagusa maisha ya maelfu ya Watanzania kwa kurejesha heshima, kuimarisha elimu na kuwawezesha wasichana kufikia ndoto zao bila vikwazo.
Huu ni ushahidi wa wazi kwamba sekta binafsi inaweza kuwa na mchango mkubwa kati ka kuleta mabadiliko yenye tija na endelevu katika jamii.