Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini, waliandamana siku ya Jumanne katika miji mbalimbali nchini humo, kushinikiza kuondoka kwa wageni wanaoishi katika nchi hiyo bila kuwa na vibali halali vya ukaazi na kufanya kazi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yamefanyika baada ya kampeni ya wiki kadhaa, kuwataka wageni hasa Waafrika wasio na vibali kuondoka nchini Afrika Kusini kufikia tarehe 30 mwezi Juni.

Kwa kiasi kikubwa maandamano hayo yalikuwa ya amani, huku polisi wakipiga doria kuhakikisha kuwa amani inakuwepo, lakini jijini Johannerburg makaazi na maeneo ya kufanyia biashara ya wageni yalishambuliwa kwa mawe.

Watu kadhaa pia walikamatwa kwa wizi kwenye maduka yanayomilikiwa na wageni, licha ya kuwepo pia kwa ulinzi wa wanajeshi katika majiji ya Johannesburg na Durban.

Raia wa Afrika Kusini wanadai kuwa, uwepo wa wageni wasio na vibali katika nchi yao, kumewasababishia ukosefu wa ajira na pia wanasababisha visa vya utovuwa wa usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *