
Nchini Niger, serikali imefunga kazi za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 2,900 kati ya 4,700 ya ndani ya nje, yanayofanya shughuli zake katika taifa hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imetangazwa na Wizara ya Mambo ya ndani, ikifuata hatua ambayo pia ilichukuliwa na nchi jirani ya Burkina Faso ambayo pia inaongozwa na wanajeshi, ambapo wiki iliyopita, ilifuta mashirika zaidi ya 100 yasiyokuwa ya kiserikali.
Nchini Niger, uongozi wa kijeshi, unadai kuwa mashirika hayo hayana uwazi katika shughuli zao na yale yaliyofutwa yamebainika kushiriliana na magaidi na hivyo, kudhoofisha usalama wa baadhi ya maeneo nchini humo.
Hii sio mara ya Kwanza kwa Niger kuchukua hatua hii, mwaka uliopita mashirika kadhaa pia yalifutwa kwa madai ya kutochapisha rekodi ya matumizi yake ya fedha, kwenye Gazeti la serikali.
Kazi za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Niger, mwaka 2024 yalisaidia kupatikana kwwa Dola Milioni 448 kutoka kwa wafadhili, kusaidia miradi mbalimbali kama ya afya, elimu hali ambayo sasa itatatizwa kwa sababu ya hatua ya uongozi wa kijeshi.