
Watu 23 wakiwemo watoto watatu, wameuwa katika mashambulizi matatu, yaliyotekelezwa na wanajihadi na watu wenye silaha, Kaskazini Mashariki na Magharibi mwa Nigeria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Washukiwa wa kundi la kigaidi la Boko Haram, limedaiwa kuwauwa watu 11 baada ya kushambulia kijiji kimoja katika jimbo la Borno, huku wengine 12 wakiuwa katika jimbo la Zamfara kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa usalama.
Ripoti zaidi zinasema, magaidi hao waliwasili katika vijiji hivyo wakiwa kwenye pikipiki kabla ya kuanza kuwapiga risasi, wanakijiji huku wengine wakiwa bado hawafahamiki waliko, huku ikihofiwa kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Matukio ya makundi ya kijihadi na kigaidi, yamekuwa yakiendelea Kaskazini mwa Nigeria kwa miaka 17 sasa, ambapo mbali na mauji, wanawateka raia wa kawaida na kudai kikombozi kabla ya kuwaachia huru.
Watalaam wa masuala ya usalama licha ya watu wenye silaha nchini Nigeria, kuendelea kutekeleza mashambulio hayo ili kupata fedha, wanaonekana kushirikiana kwa karibu makundi yenye itikadi kali kama wanajihadi wa ISWAP na kundi la kigaidi la Boko Haram.
Licha ya jeshi la Nigeria kuendelea na operesheni dhidi ya makundi hayo, Kusini Mashariki maafisa wa usalama wanalalamikia uchovu na ukosefu wa silaha za kutosha.