Tume ya umoja wa Afrika kwa nchi ya Sudan Kusini, AUMISS, imetangaza kuwa wajumbe wa baraza la usalama na amani kutoka Umoja huo, watazuru Juba kuanzia Alhamisi hadi JumamosI ya wiki hii, kufanya tathmini ya kipindi cha mpito.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, wajumbe hao watakutana na Rais Salva Kiir pamoja na viongozi wengine wa serikali, wakiwemo makamu wa rais. Pia watashirikiana na taasisi zilizoanzishwa chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, pamoja na mashirika ya kikanda kama IGAD na Tume ya pamoja ya ufuatiliaji wa usalama.

Aidha, ujumbe huo utazungumza na wadau mbalimbali kuhusu maandalizi ya uchaguzi ujao, pamoja na hatua zilizofikiwa katika kukamilisha kipindi cha mpito.

Ziara hiyo inajiri wiki chache baada ya mjumbe wa Umoja wa Afrika, Jakaya Kikwete, kuzuru nchi hiyo na kufanya mazungumzo na Rais Kiir pamoja na wadau wengine kuhusu juhudi za kurejesha amani, ikiwemo suala la wafungwa wa kisiasa akiwemo  Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar na utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha vita.

Hata hivyo, hali ya usalama nchini Sudan Kusini bado ni tete licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani mwaka 2018 kati ya Rais Kiir na Makamu wake wa kwanza Riek Machar. Machar aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani Machi mwaka jana na kuondolewa madarakani , hatua iliyoongeza mvutano ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *