
Zaidi ya wafungwa 900 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasubiri adhabu ya kifo, kulingana na takwimu kutoka kwa ripoti ya uchunguzi iliyochapishwa na mashirika kadhaa yanayopambana dhidi ya adhabu ya kifo nchini DRC. Watu hawa walihukumiwa na mahakama ingawa DRC ilifuta adhabu ya kifo mwanzoni mwa mwaka 2024.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi
Ujumbe ulioongozwa mwaka 2024-2025 na mashirika matatu yasiyo ya kiserikali yanayopambana dhidi ya adhabu ya kifo nchini DRC, unaonyesha kuzorota kwa hali ya wale waliohukumiwa kifo nchini DRC.
Ingawa ripoti hiyo inasema katika utangulizi wake kwamba mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo hajanyongwa rasmi tangu kufutwa kwa adhabu ya kifo nchini DRC, inaibua wasiwasi kuhusu idadi isiyo ya kawaida ya hukumu za kifo. Mnamomwaka 2024, angalau hukumu 480 za kifo zilitolewa na mahakama ya Kongo. Kulikuwa na 122 mwaka wa 2023. Kwa kulinganisha, kwa miaka ya 2021, 2022, na 2023, watu 153, 163, na 122, walihukumiwa adhabu ya kifo mtawalia.
Kwa hivyo, idadi ya wafungwa waliohukumiwa kifo pia imeongezeka sana. Kulingana na waandishi wa ripoti hiyo, iliongezeka maradufu kati ya mwaka 2019, mwaka wa utafiti uliopita, na mwaka 2025. Hivi sasa, watu 916 waliohukumiwa kifo wanashikiliwa nchini DRC, 300 kati yao wanazuiliwa katika gereza moja la Angenga katika mkoa wa Mongala. Gereza hili limetengwa sana, limechakaa, na halina usafi, ambapo wafungwa wanakosa maji na chakula.
Hatimaye, mashirika hayo matatu yasiyo ya kiserikali pia yanaonya kuhusu ukiukwaji wa baadhi ya taratibu za kimahakama uliosababisha hukumu hizi, yakibaini kwamba “mabadiliko yaliyofanywa na mamlaka yamebadilisha adhabu ya kifo kuwa chombo cha mawasiliano ya kisiasa.”