Umoja wa Mataifa umesema viwango vya juu vya joto vinawazuia wakulima kufanya shughuli zao za ukulima, mifugo wakitarajiwa kufariki zaidi kutokana na joto katika baadhi ya nchi duniani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ongezeko la joto linatishia mifumo ya chakula duniani, uzalishaji ukiendelea kupungua, hatua inayotarajia kuwaathiri pakubwa watu Bilioni moja.

Watalaam kutoka mashirika ya FAO na WMO wanasema wakulima huenda watatatizika kufanya shughuli zao katika kipindi cha siku 250 mwaka huu kutokana na viwango vya juu vya joto.

Wakulima walio kusini na katikati mwa Amerika, India, Asia Kusini na wale kutoka nchi zilizo kwenye jangwa la sahara ndio wanaotarajiwa kuathirika zaidi.

Tayari mifugo kadhaa wameripotiwa kufa, mimea ikiathirika  katika baadhi ya nchi ambako kumeshuhudiwa nyuzi joto za viwango vya 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *