#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Ushetu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Emmaneul Cherehani ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Nishati kuwekeza miundombinu na umeme wa uhakika katika vijiji, Kata na maeneo mengine yenye makusanyo makubwa ili watanzania waweze kufanya uwekezaji wenye tija, kuongeza mapato nakunufaika na kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Cherehani ameeleza hayo bungeni Dodoma Aprili 22, 2026 wakati Wizara ya Nishati iliposoma bajeti ya mwaka 2026/2027 ndani ya bunge hilo.

Awali ameshukuru Serikali kuputia wizara hiyo kwa kutekeleza mradi wa kufua umeme wa jua uliogharimu kiasi cha Sh bilioni 11 uliopo katiak Kijiji cha Kayenze Kata ya Ukune katika Halamashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Amesema pamoja na utekelezaji huo nado anaiomba wizara hiyo kutimiza ahadi ya kituo cha kupoozea umeme iliyompatia miaka mitatu iliyopita akifafanua kuwa amepokea vijiji 112 vina umeme tayari na katika vitongoji 554 vya kwenye Jimbo lake tayari vitongoji 285 vinaumeme na wamempa vitongoji 136 ameomba vitongoji 145 vibaki wamalizie ili wananchi waweze kunufaika na kazi za Rais Samia.

Pia amesema ameomba wizara hayo ifanikishe upatikanji wa nishati kubwa na za uhakika katika kata zenye makusanyo na mapato makubwa katika jimbo lake kwani kutokuwa na umeme wa uhakika kumekuwa kukikwamisha shughuli zao za uwekezaji na uzalishaji hususani katika eneo la Mwabomba ambalo wananchi wengi hujenga viwanda.

“Naomba mtuletee transfoma zenye uweze mkubwa mimi hapa niliomba Mkoa wa Kitanesco Kahama, alisema Kahama inahitaji mkoa wa Tanesco makusanyo ya Kahama tunakusanya zaidi ya bilioni 7.370 na kwa mwaka wanakusanya zaidi ya bilioni 90 na kwa miaka mitatu ni zaidi ya milioni 290 lakini kuna miundombinu mibovu, umeme unakatika kila mara na biashara za watanzania katika halmashauri zetu tatu imekuwa na biashara kubw asana ya jenereta kuliko kulipia umeme,” ameeleza Cherehani.

Ameongeza kuna eneo linaitwa Dodoma kuna vijana zaidi ya 3000 wametengewa eneo lao wamewekeza lakini changamoto na kilio chao ni kukatika katika kwa umeme hali ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara na mashine zao kuungua.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *