Kundi la kwanza la wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani na kupelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia kusainiwa kwa makubaliano kati ya nchi hizo mbili liliwasili mjini Kinshasa siku ya Ijumaa, Aprili 17. Kundi hilo la watu 15, kwa sasa wamewekwa katika hoteli karibu na mji mkuu wa Kongo, ambapo wanasaidiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM). Ingawa walipewa visa ya wiki moja walipowasili, sasa wanakabiliwa na chaguo: kurudi katika nchi zao za asili au kubaki DRC.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ili kukutana na wahamiaji hawa, wanaotoka Peru, Colombia, na Ecuador, mtu lazima asafiri hadi Venus Village, kilomita chache kwa gari kutoka uwanja wa ndege, nje kidogo ya mji wa Kinshasa, mbali na mjini kati.

Tulipokutana nao, walikuwa wakirudi kutoka mkutano na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM). Wanakiri kuhisi wasiwasi kidogo nchini DRC, ingawa wanaona hali yao ya maisha kuwa ya kuridhisha. “Kwa sasa, hali yangu ya maisha iko sawa: Nina chumba cha kulala, milo mitatu kwa siku, na katika hatua hii, najisikia vizuri. Siruhusiwi kuondoka kwenda popote pale ninapotaka, wala mitaani wala mahali pengine popote, lakini ndiyo, kwa sasa najisikia vizuri,” anasema Hugo Palencia. Yeye ni raia wa Colombia na ndiye aliye tayari zaidi kujadili hali yake.

Kuwasili DRC katikati ya usiku

Wengine wako tayari kuzungumza, lakini mbali na kipaza sauti na hawataki majia yao yatajwe. Wote wanasimulia kilichowasibu: kuzuiliwa katika vituo vya uhamiaji vya Marekani, tangazo la kufukuzwa kwao nchini Marekani na kutumwa DRC chini ya saa 24 kabla ya muda uliopangwa, kuondoka kwao haraka kutoka Louisiana, safari ya ndege isiyoisha na kutua mara mbili huko Dakar na Accra, kuwasili kwao katikati ya usiku katika Uwanja wa Ndege wa Ndjili katika joto kali, na kisha kupelekwa Venus Village, hoteli iliyojengwa kwa ajli ya watu kupumzikia ambayo ina bwawa la kuogelea na na uwanja wake wa tenisi uliochakaa.

Tangu wakati huo, mara chache wameondoka katika eneo hilo. “Sijui ni kwa nini Marekani inafanya makubaliano na nchi za Afrika,” Hugo amesema. “Kwa heshima yote, DRC haina maendeleo mengi kuliko Marekani au nchi zetu husika. Hapa, umaskini ni mkubwa na ukosefu wa usalama ni mkubwa kuliko Colombia, mahali ninapotoka, na ambapo hali tayari ni ngumu…”

Wahamiaji hawa wote pia walionyesha wasiwasi wao kuhusu kitakachofuata. Paola ameeleza kwamba wana hadi Ijumaa, Aprili 24, kuamua kama wanataka kubaki DRC na kuomba hifadhi nchini humo, au kama wanachagua kurudi kwa hiari katika nchi yao ya asili. Mchakato huo unaweza kuchukua miezi kadhaa. Baadhi, kama Hugo, tayari wamefanya chaguo lao: “Kusema kweli, sina nia ya kubaki DRC. Nataka kurudi nchini kwangu kumwona mwanangu, familia yangu, baba yangu, mama yangu, kwa sababu wananisubiri huko. Iwe tunaogopa au la, kwa upande wangu, nataka kurudi nchini kwangu kwa sababu, mwishowe, kwa heshima yote kwa Kongo, ninaogopa zaidi kuwa hapa kuliko Colombia.” “

Maamuzi ya mahakama ambayo hayajaheshimiwa

Kwa kuwasiliana na mamlaka huko Bogotá, sasa anasubiri hati ziondoke haraka iwezekanavyo: “Ninasubiri hati ya kusafiria. Nataka Wizara ya Mambo ya Nje au ubalozi mdogo wa Colombia kuwasiliana na shirika linalotusimamia haraka iwezekanavyo. Tuliona taarifa kutoka kwa rais wetu, Gustavo Petro, ambaye anataka turudi haraka iwezekanavyo.”

Lakini Hugo bado anahisi hasira kuhusu kilichompata. Anabainisha kwamba nchini Marekani, alilindwa na uamuzi wa mahakama uliyotolewa muda mfupi kabla ya kufukuzwa kwake. Sio yeye pekee aliye katika hali hii: Paola pia anaelezea kwamba yuko katika hali kama hiyo. Kisha Hugo akasema hakuelewa jinsi mamlaka ya uhamiaji ya Marekani iliweza kumpeleka Kinshasa bila idhini yake na licha ya uamuzi wa jaji wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *