Nchini Mali, jeshi limesema limepambana na  makundi ya kigaidi, yaliyoshambulia jiji kuu Bamako na viunga vyake, siku ya Jumamosi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Walioshudia mashambulizi hayo wanasema, yalitokea na karibu na makaazi ya kiongozi wa kijeshi Jenerali Assimi Goita, ambako milio mikubwa ya silaha ilisikika.

Taarifa ya jeshi, imesema makundi ya kigaidi ambayo haikutaja, yalishambulia kambi kadhaa za jeshi jijini Bamako na miji mingine kama Gao na Kidal.

Helikopta za kijeshi zimeonekana katika angaa la Bamako, huku zikizunguka uwanja wa Kimataifa wa ndege, huku mapigano makali  yakiripotiwa.

Waasi wa Tuareg, wamedai kuhusika pia na mashambulizi yaliyotokea mjini Kidal, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Tangu mwaka 2020, Mali imekuwa ikiongozwa na wanajeshi baada ya utawala kiraia kuondolewa na tangu kipindi hicho, uongozi wa nchi hiyo umeendelea kupambana na makundi ya kijihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *