
Mazungumzo kati ya Marekani na Iran ili kukomesha vita yanatarjiwa kuanza tena leo Jumamosi Aprili 25, huku wajumbe kutoka pande zote mbili wakisafiri hadi Islamabad, ingawa majadiliano ya moja kwa moja hayana uhakika, wiki mbili baada ya jaribio la awali kushindwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wajumbe wa Donald Trump, Steve Witkoff na Jared Kushner, pia wanatarajiwa kwenda Pakistan Jumamosi, Aprili 25, ingawa hakuna mkutano kati ya pande hizo mbili uliopangwa rasmi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi aliwasili Islamabad siku ya Ijumaa jioni kwa mazungumzo na maafisa wakuu wa Pakistan. Lakini “hakuna mkutano uliopangwa kati ya Iran na Marekani,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baghai alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, akiongeza kuwa msimamo wa nchi yake utawasilishwa kwa upande wa Marekani kupitia wapatanishi wa Pakistan.
Wajumbe wa rais Donald Trump, Steve Witkoff na Jared Kushner, watasafiri kwenda Pakistan siku ya Jumamosi kwa mazungumzo “na wawakilishi wa ujumbe wa Iran,” msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alisema mapema, akibainisha kwamba mkutano huo ni ombi la Tehran.
Makamu wa Rais JD Vance, ambaye aliongoza ujumbe wa Marekani wiki mbili zilizopita, hatarajiwi wakati huu kuwa sehemu ya timu ya ujumbe wa Marekani lakini anaweza kujiunga nao baadaye ikiwa maendeleo yatapatikana, Leavitt aliongeza.