Rais wa Marekani Donald Trump, Makamu wake JD Vance na maofisa wengine wa serikali walikimbizwa katika eneo salama baada ya milio ya risasi kusikika kwenye ukumbi ambapo walikuwa wakihudhuria halfa moja jijini Washington usiku wa kuamkia leo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na video zilizonaswa kutoka kwenye eneo ambalo tukio hilo limetokea, maofisa wa usalama wanaonekana wakimuondoa kwa dharura Trump pamoja na JD Vance baada ya milio ya risasi kusikika, wengine waliokuwemo pia wakihamishiwa kwenye eneo salama.
Mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha, alijaribu kupita kizuizi cha walinda usalama nje ya ukumbi ambapo halfa hiyo ilikuwa ikifanyika kabala maofisa wa usalama mwa Marekani kumzindia nguvu.
Wageni wengine wanaonekana wakijificha chini ya meza wakati vurugu zilipoaanza. Baada ya tukio hilo Rais Trump amethibitisha kuwa mshukiwa aliyekuwa amejihami kwa bastola amekamatwa, akichapisha picha zake kwenye mitandao yake ya kijamii.
Aidha Rais Trump amethibitisha kuwa afisa mmoja wa ulinzi wa Marekani alipigwa risasi kwa karibu wakati wa tukio hilo japokuwa hakujeruhiwa vibaya.
Licha ya kutokea kwa tukio hilo la kufytatua risasi, Rais Trumo amesisitiza kuwa atapanga tena halfa nyengine na wanahabari wanaofanya kazi katika Ikulu ya White House katika kipindi cha mwezi mmoja.
Trump aliwahi kulengwa katika jaribio la mauaji wakati akiwa kwenye mkutano huko Butler, Pennsylvania mnamo 2024.
Miezi michache baadaye, mtu mwingine alikamatwa na walinzi wa Trump akiwa na nia ya kumuuwa wakati alipokuwa akicheza gofu kwenye uwanja wa gofu wa West Palm Beach.
Katika eneo la Washington Hilton ambapo hafla ya hapo jana Jumamosi ilifanyika ilikuwa mahali ambapo Rais wa Republican Ronald Reagan alipigwa risasi na mtu aliyekuwa na nia ya kumuua mnamo 1981.