
Chombo cha habari cha Kizayuni kimeripoti ongezeko kubwa la idadi ya kujiua katika jeshi la utawala wa Kizayuni tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2026.
Gazeti la Haaretz limekiri katika ripoti yake kwamba kujiua miongoni mwa wajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Iirael kumeongezeka tangu mwanzo wa 2026. Ripoti hiyo inasema, zaidi ya wanajeshi 11 wa Israel wamejiua tangu mwanzo wa mwaka huu. Ripoti hiyo imeashiria ongezeko kubwa la kujiua wanajeshi wa Israel mwezi huu wa Aprili, ambapo visa 6 vikirekodiwa katika jeshi pekee.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza Oktoba 7, 2023, visa vya matatizo ya akili vimeongezeka katika jeshi la Israel, na tangu 2025 pekee, visa 21 vya kujiua na majaribio 279 ya kujinyonga yamerekodiwa miongoni mwa wanajeshgi wa utawala huo.
Pia, ripoti kutoka Kituo cha Utafiti cha Bunge la Israel zinaonyesha kwamba asilimia 78 ya visa vyote vya kujiua vilivyorekodiwa huko Israel mwaka wa 2024 vilihusiana na jeshi. Idadi hii ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, na inaakisi athari za moja kwa moja za vita kwa afya ya akili ya Wazayuni.