Rasimu hii inayolenga kuingiza dhana ya ridhaa katika sheria ya ubakaji ya nchi 27 wanachama wa EU itapigiwa kura na wabunge wa Ulaya leo Jumanne, Aprili 28, huko Strasbourg. Ingawa pendekezo kama hilo tayari lilipitishwa na taasisi hiyo miaka miwili iliyopita, baadaye lilizuiwa na nchi kadhaa—ikiwa ni pamoja na Ufaransa—katika ngazi ya Baraza la Ulaya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa Ulaya watapiga kura Jumanne, Aprili 28, kuhusu rasimu inayolenga kulazimisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kurekebisha sheria zao ili kujumuisha dhana ya ridhaa katika sheria zao za ubakaji na kuharamisha kitendo chochote cha ngono ambapo hakuna ridhaa huru na inayoweza kubatilishwa. Ingawa baadhi ya nchi, kama vile Sweden, Uhispania, na Denmark, tayari zimeingiza dhana hii kwenye sheria zao, zingine zimechelewa sana.

Mbunge wa Sweden na mwandishi wa nakala hii, Evin Incir, anaona uwasa huu ni muhimu. “Sio nchi zote wanachama zina sheria sawa. Ikiwa maandishi haya yatapitishwa, yatamaanisha kwamba wanawake katika nchi 27 za EU wanaungwa mkono katika kukabiliana na ubakaji,” anaelezea, akisisitiza kanuni moja: “‘Ndiyo’ pekee inamaanisha ndiyo. Kila kitu kingine kinamaanisha hapana!”

Pendekezo ambalo tayari limepigiwa kura lakini limezuiwa katika Baraza la Ulaya

Bunge la Ulaya lilikuwa tayari limeshughulikia suala hili miaka miwili iliyopita, likipitisha pendekezo kama hilo kwa wingi mkubwa. Lakini nakla hiyo ilizuiwa katika Baraza la Ulaya, haswa na Ufaransa, Ujerumani, na Hungary.

Hata hivyo, leo, Evin Incir ana matumaini zaidi, kwa sababu muktadha umebadilika. “Tangu wakati huo, nchi wanachama wa EU zimeanza kurekebisha sheria zao za kitaifa,” anabainisha, akitoa mfano wa Ufaransa, ambayo imekuwa na sheria inayotegemea ridhaa tangu vuli ya mwaka 2025, na kubainisha kwamba Italia inahusika katika mchakato kama huo. Kwake, “wakati umwadia sasa!”

Ingawa nakala hiyo inatarajiwa kupata wingi tena katika Bunge, kupitishwa kwake kwa mara ya mwisho kutategemea tena Baraza la Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *