Nchini Mali, wanajihadi wanaoshirikiana na waasi wa Tuareg, wameuteka mji wa Kidali Kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, kutekeleza mashambulizi makubwa katika maeneo mbalimbali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii imekuja baada ya siku mbili za mapigano makali, kati ya wanajihadi hao na wanajeshi, hali ambayo imezua maswali kuhusu udhabiti wa uongozi wa kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Mashambulizi ya wanajihadi hao, yalisababisha kifo cha Waziri wa Ulinzi Jenerali Sadio Camara, wakati huu kiongozi wa kijeshi Jenerali Assimi Goita, ambaye alichukua madaraka mwaka 2020, akiwa hajaonekana wala kuzungumza.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Abdoulaye Maïga amejitokeza na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa kwenye uwanja wa mapambano na kuwahakikishia wananchi kuwa, utawala wa kijeshi unarejesha hali ya kawaida nchini humo.
Jiji kuu Bamako na miji mingine ya kimkakati yalilengwa na shambulizi hilo la wanajihadi na waasi, kitendo ambacho wachambuzi wa masuala ya ulinzi na usalama ni changamoto kubwa kwa nchi hiyo.