
Mlipuko wa virusi vya Ebola unaendelea kuenea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nchi hiyo sasa ina wagonjwa 875 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola, ikiwa ni pamoja na vifo 202, kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magojwa, Africa CDC, shirika la afya la Umoja wa Afrika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hali nchini Uganda bado haijabadilika. Ituri inabaki kuwa kitovu cha janga hilo ikiwa na wagonjwa 799 waliothibitishwa. Lakini hali katika mkoa wa Kivu Kaskazini inatia wasiwasi, kulingana na Africa CDC.
Ingawa Kivu Kaskazini ina wagonjwa 73 pekee waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola, kiwango cha vifo—yaani, idadi ya vifo ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa—ni kubwa zaidi, na kufikia 59%. Na shirika la afya la Umoja wa Afrika, Africa CDC, lina wasiwasi. Ukosefu wa usalama katika mkoa huu wa DRC unazuia mwitikio wa kweli kwa janga hili, kulingana na Dkt. Wessam Moukala.
“Usalama ni changamoto kubwa. Unapunguza harakati za timu zetu, ambazo haziwezi kuwafikia raia, kufanya kazi ya kuzuia, kuangalia wagonjwa wanaoshukiwa kuambukizwa na kuwatenga ikiwa ni lazima, pamoja na kutambua na kufuatilia watu waliotanfamana nao,” anaelezea.
Kivu Kaskazini ina kiwango cha chini kabisa cha ufuatiliaji na utambuzi wa waliotangamana na wagonjwa miongoni mwa mikoa mitatu iliyoathiriwa na janga hili, kulingana na shirika la afya, ambalo pia lina hofu kwamba kutokana na ugumu wa kufikia katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo, idadi halisi ya wagonjwa inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko inavyoripotiwa sasa. Africa CDC inatoa wito kwa mamlaka mbalimbali kuzipa timu zake ufikiaji wa haraka katika maeneo haya ili kuimarisha mwitikio wa kiafya.