‎#HABARI: Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa kushirikiana na taasisi ya Qatar Charity, imezindua kambi maalum ya siku sita ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wa Dar es Salaam.

Bingwa bobezi wa magonjwa ya kisukari, Dkt. Joseph Minja, ameeleza kuwa kambi hiyo inalenga kupambana na ongezeko la magonjwa kama kisukari na shinikizo la juu la damu kwa kutoa vipimo, elimu, na dawa bila malipo kwa lengo la kuimarisha afya ya jamii.

Huduma hizo zimegawanywa katika awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inafanyika katika uwanja wa Zakhem, Mbagala kuanzia Aprili 28 hadi 30, kabla ya kuhamishiwa Kigamboni kwa siku tatu zilizobaki.

Utaratibu huu unalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo yao ili kuwarahisishia utambuzi wa mapema wa magonjwa hayo, jambo ambalo ni muhimu katika kuzuia madhara makubwa ya kiafya yanayoweza kuepukika kupitia matibabu ya dharura.

Mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi katika siku ya kwanza pekee ya uzinduzi wa kambi hiyo mkoani Dar es Salaam.

Dkt. Minja amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata ushauri wa kitaalamu na dawa, akisisitiza kuwa utambuzi wa mapema unasaidia kupunguza gharama za matibabu ya muda mrefu na kuokoa maisha ya Watanzania wengi wanaokabiliwa na changamoto hizo za kiafya.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *