
Juhudi za kukomesha vita nchini Iran zimefikia kikomo. Rais wa Marekani, akiwa hajafurahishwa na pendekezo la hivi karibuni la Iran, amesema siku ya Jumanne, Aprili 28, kwamba Tehran iliifahamisha Marekani kwamba Iran iko karibu ya kuanguka na inataka kufutwa kwa kizuizi cha baharini cha Marekani. Rais wa Marekani amewaomba washauri wake kujiandaa kwa ajili ya kizuizi cha kijeshi kwa muda mrefu dhidi ya Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani Donald Trump amewaomba washauri wake kujiandaa kwa ajili ya kuendelea na kizuizi kwa muda mrefu dhidi ya Iran, linaripoti Gazeti la Wall Street Journal (WSJ), likiwanukuu maafisa wa Marekani.
Katika mikutano ya hivi karibuni, rais wa Marekani aliamua kuendelea kuweka shinikizo kwa uchumi wa Iran na mauzo ya nje ya mafuta kwa kuzuia shughuli zote za baharini kwenda na kurudi kutoka bandari zake, kulingana na gazeti hilo. Donald Trump anabainisha chaguzi zake zingine, ikiwa ni pamoja na kuanza tena kwa mashambulizi au kujiondoa kwenye mzozo, zina hatari zaidi kuliko kudumisha kizuizi hicho, linaripoti WSJ.
Kulingana na Wall Street Journal, ikinukuu vyanzo visivyo rasmi ndani ya utawala wa Marekani, Donald Trump anapendelea hali ilivyo: kizuizi cha muda mrefu cha Mlango-Bahari wa Hormuz, badala ya chaguzi nyingine mbili zinazopatikana kwake, kuanzishwa kwa tena kwa mashambulizi au kujiondoa kwenye mzozo, anaelezea mwandishi wetu wa Washington, Vincent Souriau.
Kulingana na gazeti la kila siku la New York, Ikulu ya Marekani inaamini kizuizi hicho kina athari za haraka. Inaripotiwa kwamba Iran ina mafuta mengi ambayo hayajauzwa na haina uwezo wa kuyahifadhi, huku mapato ya utawala yakishuka. Kulingana na vyanzo vilivyo karibu na rais wa Marekani, shinikizo hili ndilo lililowafanya viongozi wa Iran kupendekeza mpango mpya wa mazungumzo wa hatua tatu, ambao Washington imekataa hadi sasa, huku Donald Trump akisisitiza kuhusu mpango unaojumuisha mpango wa nyuklia wa Iran, pamoja na kusitishwa kwa angalau miaka 20 kwa urutubishaji wa uranium.