Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa pole kwa familia ya Anna Maulida Komu huku kikisema kitamkumbuka kwa kwa rekodi mbalimbali ikiwemo ya kuwania ugombea mwenza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Kimesema jana Jumatano, Aprili 29, 2026 kilishindwa kutoa kauli kutokana na vikao vya kamati huu, lakini kiliwatuma Dk Azaveli Lwaitama (makamu mwenyekiti wa bodi) na Said Mzee Said (makamu mwenyekiti Chadema Zanzibar), kushiriki maziko.

Maulida Komu ambaye hadi umauti unamfika Jumanne usiku alikuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chadema, alizikwa jana Jumatano Mjini Unguja, huku baadhi ya watu waliowahi kufanya naye kazi wakimkumbuka wa kupigania haki.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Amani Golugwa amesema leo Alhamisi Aprili 30, 2026 chama hicho kinachotambua hadi Maulida anafariki alikuwa mwanachama wao na mjumbe wa bodi ya wadhamini.

“Hadi anafariki alikuwa alikuwa rekodi ya kuwa mgombea mwenza wa urais mwaka 2005 akiiwakilisha Chadema, pia alikuwa na kesi ya kukishtaki chama na kusababisha Chadema kufungiwa,” amesema Golugwa.

Mwaka 2025, Maulid wajumbe wengine wa bodi ya wadhamini ya Chadema, Ahmed Rashid Khamis na Said Issa Mohamed, walifungua kesi ya mgawanyo wa mali za chama hicho.

Katika kesi hiyo, waliomba mahakama izuie Chadema kufanya shughuli za kisiasa,pia mhimili huo ulizuia mali za chama hicho zisiguwe, hatua iliyosababisha ofisi na magari kukaa kwa muda mrefu bila kutumika.

Golugwa amesema pamoja na Maulida Komu kuwa narekodi nyingi lakini Chadema hakitamsahau kwa namna alivyofungua kesi hiyo yeye, Said Issa na mwenzao akisema litakuwa katika kumbukumbu.

“Hatuna mengi ya kusema tunatoa pole kwa familia, lakini hatuna lolote zaidi ya haya niliyoyasema,” amesisitiza Golugwa.

Kwa mujibu wa Salum Mwalimu ambaye ni ndugu wa Maulida Komu, amesema mama yake mkubwa huyo alilazwa hospitalini Unguja kwa takribani wiki tatu kabla ya kufikwa na umauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *