Mahakama Kuu nchini Uganda, imemkuta na hatia Christopher Okello Onyum, na kumuhukumu kunyongwa kwa makosa manne ya mauaji ya watoto wanne wa shule katika Kituo cha Maendeleo ya Watoto wa Awali cha Ggaba, April 2 mwaka huu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akisoma uamuzi wake, Jaji Alice Komuhangi Khaukha, amesema mtuhumiwa alitekeleza mauaji hayo katika njia ya kutisha, bila huruma wala kujali uhai wa binadamu.

Jaji Alice alitupilia mbali maombi ya utetezi kuwa Okello wakati akifanya uhalifu huo alikuwa amerukwa akili.

Mahakama imesema upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi usio na mashaka kuthibitisha namna mtuhumiwa alipanga na kisha kutekeleza uhalifu wake, akigusia historia ya mtandaoni ya mtuhumiwa ambaye imebainika alitafuta maandiko ya namna ya kutekeleza mauaji kwa kuchinja kama Kundi la Islamic State linavyofanya.

Wakati wa kusomwa kwa huku hiyo, mamia ya wakazi na wazazi wa waliopoteza Watoto wao, walikuwa wamejaa mahakamani hata kabla ya uamuzi wenyewe kusomwa katika moja ya kesi ambayo iligusa na kuamsha hisia kali za raia wa Uganda.

April mbili mwaka huu, mtuhumiwa Okello alifika katika shule ya Ggaba akiwa na kisu na kuanza kuwadunga Watoto kiholela, tukio lililosababisha vifo vya Watoto Etuku Gideon; Keisha Agenorwoth, Ignatius Sseryange na Ryan Odeke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *