Wakati wafanyakazi nchini wakiungana na wenzao duniani kote kupongezana kwa mafanikio ya utendaji kazi, hali imekuwa tofauti mkoani Geita, ambapo Baraza la Madiwani wa Chato limeazimia kuwafukuza kazi watumishi saba kutoka Idara ya Afya baada ya kubainika kukiuka taratibu za utumishi.
Aidha, watumishi wengine watatu wamepewa adhabu ya kukatwa asilimia 15 ya mshahara wao kwa muda wa miaka mitatu kufuatia uchunguzi kubaini makosa ya kiutumishi, ikiwemo utovu wa nidhamu na utoro kazini.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)