Tani 4.8 za bidhaa za maziwa ya watoto aina ya SMA namba 1 zimeteketezwa Zanzibar baada ya kubainika kuwa si salama kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuathiriwa na bakteria.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Kusini Unguja, Afisa Uhusiano wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZFDA), Fatuma Makame Juma, amesema bakteria hao wanaweza kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuumwa na tumbo, kichefuchefu na kutapika iwapo mtu atatumia bidhaa hiyo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *