BAADA ya kuenea tetesi za huenda Kiungo wa Taifa Stars, Alphonce Mabula akaondoka Shamakhi FC ya Ligi Kuu ya Azerbaijan mwishoni mwa msimu, amesema bado anatafakari kuhusu ofa zinazokuja mezani.

Inaelezwa Kasimpaşa S.K ya Ligi Kuu Uturuki na Yanga ya Tanzania zimegonga hodi kwa kiungo huyo fundi kusaka saini yake kwa ajili ya kuwa naye msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mabula amesema  kuna timu zimeonyesha nia ya kumhitaji, lakini bado hajafanya maamuzi, akiendelea kuangalia ipi itamfaa.

MABU 02

“Ngoja tuone itakuwaje, lakini timu nyingi zimenifuata. Muhimu naangalia kazi yangu, pia lazima pesa iwepo,” amesema kiungo huyo na kuongeza;

“Kila mchezaji ana malengo yake, natamani sana  niliyoyapanga yatimie na nafikiri kwa kiwango hiki inaweza kuwa tiketi ya kucheza Ulaya.”

Kiungo huyo ameendelea kuonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge na Shamakhi na msimu huu tayari amecheza mechi 25 akifunga mabao mawili.

MABU 01

Ikumbukwe mchezaji huyo amebakiza mkataba wa mwezi mmoja na timu hiyio utakaotamatika June 30 mwaka huu.

Chanzo kimoja kililipenyezea Mwanaspoti, hadi sasa Kasimpasa ya Uturuki imempelekea ofa ya zaidi ya Sh2 bilioni ili kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *