KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda, amekiri kupitia wakati mgumu kwa sasa, baada ya kushuhudia kikosi hicho kikicheza mechi 10 mfululizo za Ligi Kuu bila ya ushindi tangu mara ya mwisho kishinde Januari 31, 2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda amesema kwa sasa ni kipindi cha mpito kinachoikumba tu timu hiyo, ingawa mojawapo ya changamoto iliyopo ni baada ya washambuliaji wa kikosi hicho kuandamwa na ukame wa mabao, jambo ambalo ni la kawaida.

“Unaposhindwa kufunga basi usiruhusu mpinzani wako akakufunga. Ni kweli tumekuwa na wakati mgumu kwa sasa, lakini kama ambavyo tunajua ligi ni mbio ndefu na bado tuna mechi za kurekebisha kasoro mbalimbali zilizopo,” amesema Mgunda.

NAMU 01

Mara ya mwisho kwa timu hiyo kushinda katika Ligi Kuu Bara ilikuwa ni ushindi wa bao 1–0 dhidi ya KMC FC, Januari 31, 2026. Kuanzia hapo imecheza mechi 10 mfululizo bila ushindi, huku kati ya hizo ikichapwa tano na kutoka sare tano.

Katika mechi hizo 10 ilizocheza bila ya ushindi, Namungo imekuwa haina balansi nzuri ya maeneo yote mawili, ambapo safu ya ushambuliaji ya timu hiyo imefunga mabao manane tu, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 15.

NAMU 01 (1)

Kwa ujumla timu hiyo imecheza mechi 20 za Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kati ya hizo imeshinda tano, sare nane na kupoteza saba ikiwa nafasi ya tisa na pointi 23 huku kikosi hicho kikifunga mabao 17 na kuruhusu 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *