WINGA wa TRA United, Ramadhan Salum ‘Chobwedo’, amefikisha mabao mawili katika Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na kikosi hicho, lakini moja ya jambo la kufurahisha au kushangaza ni kwamba yote ameyafunga dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons.

Bao lake la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu huu aliifunga Prisons dakika ya 54 katika ushindi wa 1–0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, Novemba 22, 2025.

Nyota huyo akaendeleza tena rekodi ya kuifunga Prisons msimu huu ambapo alifunga bao lake la pili katika ushindi wa 3–0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Mei 1, 2026.

CHOBWE 01

Katika mechi hiyo, Chobwedo alifungua ukurasa wa mabao dakika ya pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Prisons, Edward Mwakyusa, huku mengine yakifungwa na Joseph Akandwanaho dakika ya 62 na Khassimuh Mugoya dakika ya 73.

Akizungumzia kiwango cha Chobwedo, Kocha wa TRA United, Mrundi, Etienne Ndayiragije amesema ushirikiano mzuri wa nyota huyo na wachezaji wenzake ndio siri ya kuonekana bora, kwa sababu bila ya hivyo asingeweza kutimiza majukumu yake vizuri.

CHOBWE 02
CHOBWE 02

“Katika timu kila mmoja ana ubora wake unaomtofautisha na mwingine, ila wanategemeana kwa sababu huwezi pia kucheza peke yako uwanjani. Anachoendelea kukionyesha ni jitihada nzuri kwa manufaa ya klabu na yeye mwenyewe,” amesema Ndayiragije.

Ushindi huo kwa TRA United umeifanya kusogea kutoka nafasi ya saba hadi ya tano kwa kufikisha pointi 30, baada ya kucheza mechi 20, ambapo kati ya hizo imeshinda nane, sare sita na kupoteza pia sita, ikifunga mabao 23 na kuruhusu 18.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *