Mkuu wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, amekataa ombi la maafisa wa Canada la kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mark Carney baada ya wajumbe wa Iran kuvunjiwa heshima na maafisa wa mpaka wa Canada.

Tukio hilo lilisababisha Iran kuwa nchi pekee iliyokosa kuhudhuria mkutano mkuu wa FIFA kati ya wanachama 211 wa shirikisho hilo huko Vancouver siku ya Alhamisi, huku ujumbe wote wa Iran ukikatisha safari na kurudi nyumbani.

Akisimulia sababu zilizopelekea kukatishwa safari ya ujumbe wa Iran nchini Canada, Amirmahdi Alavi, msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Iran (FFIRI), amesema: “Walipoingia nchini Canada, wenyeji waliwahoji wanachama wa ujumbe wa Iran kwa saa nyingi kwa njia isiyo na heshima.”

Amesema mkuu wa FFIRI, Mehdi Taj aliulizwa swali la kukera kuhusu moja ya matawi ya jeshi la Iran yenye fahari kubwa, ikiwa ni kielelezo cha wazi cha hatua ya Canada ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha nyeusi hapo mwaka 2024 kama “shirika la kigaidi.”

“Mkuu wa Shirikisho la Soka la Iran alijibu kwa kauli nzuri na ya kutafakarisha wengi, akitangaza kwamba Iran ina wanachama milioni 90 wa IRGC, ambao wote wanaiunga mkono nchi yao kwa fahari,” amesema Alavi.

Mehdi Taj alikuwa safarini huko Canada kwa ajili ya masuala ya michezo kama Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Asia (AFC).

Alavi amepinga vikali maelezo ya serikali ya Canada kuhusu vikosi vya usalama vya Iran.

“Neno ‘gaidi’ linawahusu wale ambao, katika uvamizi mkali dhidi ya nchi yetu, wameua shahidi karibu wanafunzi 186 katika Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebah huko Minab, mashahidi ambao hatuwezi kuwasahau, akiwemo mpendwa Makan Nasiri, aliyekuwa na umri wa miaka saba ambaye hadi sasa mwili wake haujapatikana,” amesema Alavi.

Alavi ameongeza kwamba wakati ujumbe wa Iran ulipokuwa Istanbul njiani kurudi nyumbani, Katibu Mkuu wa FIFA, Mattias Grafstrom alimpigia simu Taj mara mbili au tatu kupitia kiungo cha video akilaani vitendo vya Canada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *