
Makubaliano ya kusitisha vita kwa muda kati ya Iran, Israel na Marekani yameonekana kugonga mwamba Jumatatu baada ya pande hizo hasimu kushambuliana kwenye mlango wa bahari wa Hormuz huku taifa la Falme za Kiarabu nalo likiripoti kushambuliwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mara ya kwanza tangu makubaliano ya kusitisha vita mwezi mmoja uliopita, nchi ya Falme za Kiarabu, mshirika wa karibu wa Marekani, imeripoti kushambuliwa na Iran, ambayo ilikuwa ikilenga mojawapo ya vituo vyake vya nishati.
Mashambulio haya yanajiri siku moja baada ya rais wa Marekani, Donald Trump, kutishia kuwa Iran itaondolewa kwenye ramani ya dunia iwapo itathubutu kushambulia meli za Marekani kwenye mlango wa bahari wa Hormuz, huku Iran pia ikikanusha madai ya Marekani kwamba ilikuwa imezamisha meli zake sita.
Kutokana na kurejelewa kwa mashambulio hayo, bei ya mafuta katika soko la kimataifa imeripotiwa kupanda kwa asilimia 5, wakati huu hatima ya mazungumzo ya kutafuta suluhu la kudumu ikikosa kujulikana, Masuala mawili makuu yakitajwa kuwa chanzo moja ni mpango wa nyuklia wa Iran na jingine ni kufungwa kwa mlango wa bahari wa Hormuz, jambo ambalo Iran imeendelea kushikilia.