Wafugaji kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefanya ziara katika viwanja vya Agave, Ubena Zimozi, Chalinze mkoani Pwani, ambako kunatarajiwa kufanyika maonyesho na mnada wa kimataifa wa mifugo Juni 19 hadi 21, 2026.
Ziara hiyo imelenga kuwajengea uwezo wafugaji juu ya mbinu bora za ufugaji wa kisasa, ikiwemo lishe bora, uzalishaji na usimamizi wa mifugo kwa tija.
Meneja wa Agave, Amani Sembeta, amesema washiriki wamepata fursa ya kujifunza kwa vitendo kutoka kwa wataalamu na wafugaji wabobezi ili kuongeza ufanisi katika shughuli zao.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Kilimo wa Benki ya NMB, Robert Samini, amesema udhamini wa benki hiyo unalenga kuwaunganisha wafugaji na elimu pamoja na fursa za kifedha zitakazosaidia kukuza sekta ya mifugo.
✍ Mariam Songoro
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)