- Dkt. Daniel Odhiambo Dondi alishambuliwa vibaya kutokana na mzozo wa ardhi katika nyumba ya mababu zake ya Kijiji cha Kabong’o katika kaunti ya Homa Bay
- Mashahidi waliripoti matukio ya taharuki huku binti wa Dondi akiwaarifu majirani wakati wa tukio hilo lililosababisha baba yake kukatwakatwa hadi kufa bila huruma
- Mzozo wa ardhi unaoendelea ulisababisha kifo cha msomi huyo mashuhuri wa Chuo Kikuu cha Maseno na sasa baba yake ameelezea kilichotokea
Homa Bay, Kenya: Baba wa marehemu Dkt. Daniel Odhiambo Dondi ameshiriki kwamba alijifunza kwamba mwanawe alikuwa katika matatizo mengi baada ya mjukuu wake kuanza kupiga kelele, na alipofika huko, alikuwa tayari amekufa.

Source: Facebook
Daniel alishambuliwa vibaya sana katikati ya mgogoro wa ardhi unaoendelea uliomkabili na jirani yake wa karibu, na mashahidi waliripoti kwamba binti wa profesa wa Chuo Kikuu cha Maseno alikimbia na kuwaarifu majirani, na kusababisha mshukiwa kutoroka.
Watu walipokaribia boma ili kuona kinachoendelea Familia ya Dondi ilizungumza kwa kina kuhusu mgogoro wa muda mrefu kuhusu ardhi ambao hatimaye uligharimu maisha ya msomi mashuhuri.

Pia soma
Magazeti ya Kenya, Julai 1: NTSA sasa yafyata mkia kuhusu sheria ya ukaguzi wa lazima wa magari
“Nilimsikia binti yake akilia na kulia yapata saa kumi na mbili, kwa hivyo nilimpigia simu mkwe wangu na kumuuliza kwa nini Terry alikuwa akilia sana,” alisema baba yake mzee.
“Nilidhani alikuwa akiadhibiwa na baba yake lakini nilipokaribia eneo la tukio, nilishtuka kumuona amekufa; aliuawa, akakatwa shingo,” aliongeza baba mzee.
Familia ya Dondi ikoje baada ya kifo?
Baba aliyekuwa akiomboleza alipozungumzia kifo cha mwanawe, watu waliweza kusikika wakilia kwa uchungu nyuma, na watu wengi waliotazama video hiyo pia walisema kwamba waliathiriwa na vilio hivyo, ambavyo vilionyesha maumivu makali ya familia.
Watumiaji wa mtandao walimfariji mwanamume huyo, huku wakishiriki matukio kama hayo ambayo yalisababisha mvutano mwingi katika familia zao na, katika baadhi ya matukio, kusababisha vifo vya wapendwa wao.
Wakenya walisema nini kuhusu video hiyo?
Pamela Omondi:
“@Pamela Omondi:jojuogiiiiiiiiiiiiiii anyuolaaaaaa😭😭😭.”
Brooklyn Carols
“God uko wapi to help.”
It’s LILLY 🇰🇪📌🦚💜
“The background’s sound 🥺💔💔😭😭😭😭 Mimi nae home hapna 🙌🙌🙌 story na land zea.”
Dada Eunice
“Poleni sana, Mungu awape nguvu aki niuchungu sana baba wabinguni ndiye mlipa kisasi muwachieni atawalipzia poleni.”
Pamela Omondi:
“@Pamela Omondi:jojuogiiiiiiiiiiiiiii anyuolaaaaaa😭😭😭.”
Brooklyn Carols
“God uko wapi to help
It’s LILLY 🇰🇪📌🦚💜:
“The background’s sound 🥺💔💔😭😭😭😭 Mimi nae home hapna 🙌🙌🙌 story na land zea.”
Dada Eunice:
“Poleni sana. Mungu awape nguvu aki niuchungu sana baba wabinguni ndiye mlipa kisasi muwachieni atawalipzia poleni”
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
