Wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) wamewahimiza wanafunzi wa vyuo mbalimbali kuchagua taaluma ambazo uwanda mkubwa wa kuajiri na kujiajiri.

Akizungumza katika kongamano la wahitimu hao (alumni), Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere, Mercelina Chijoriga amesema hilo linaendana na kuzingatia mafunzo ya vitendo ili kuendana na kasi ya teknolojia.

Na kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Edda Tandi Lwoga amesema kukutana na wahitimu hao kunasaidia kufanikisha uwepo wa mitaala inayoendana na wakati kutokana na uzoefu walionao wahitimu hao.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *