Watalaam wa afya wanasema ongezeko la maambukizi ya virusi vya hanta nchini Argentina, ambako meli ya kitalii MV Hondius ilitia nanga, inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika la afya duniani WHO linasema mpaka sasa nchi hiyo ya Kusini mwa Amerika, inaongoza kwa idadi ya maambukizi, wakati huu uchunguzi unapoendelea kubaini iwapo Argentina, ndio chimbuko la virusi hivyo.

Aidha, watalaam wa afya wanafuatilia ripoti kuwa, kuna kundi la abiria waliokuwa wameambukizwa na walishukia katika kisiwa cha Saint Helena, Kusini mwa Bahari ya Atlantic.

Meli ya MV Hondius ikipita katika bandari ya Praia nchini Capverde
Meli ya MV Hondius ikipita katika bandari ya Praia nchini Capverde REUTERS – Stringer

WHO inasema watu hao walioshuka katika meli hiyo ni kutoka mataifa 12 yakiwemo Uingereza na Marekani, na nchi zao zimefahamishwa.

Katika hatua nyingine, Daktari Karin Ellen Veldkamp, kutoka chuo cha utafiti wa magonjwa nchini Uholanzi, amesema mlipuko wa ugonjwa huo hausambai kama ule wa Uviko 19.

WHO inasema haitarajii virusi hivyo kusambaa, iwapo hatua za kiafya kuzuia maambukizi hayo kati ya binadamu, zitazingatiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *