#HABARI: Zaidi ya wananchi 683,767 katika Mkoa wa Dodoma wamefikiwa na kunufaika na huduma za msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Kitaifa ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign), inayotekelezwa na Serikali chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Akitoa tathmini ya utekelezaji wa kampeni hiyo leo Jumamosi, Mei 09, 2026, jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria, Bi. Esther Msambazi amesema mafanikio hayo ni kielelezo cha kiu ya wananchi kupata haki na elimu ya sheria nchini.
Katika tathmini hiyo, Bi. Msambazi amebainisha kuwa kampeni hiyo inaendelea pia katika Mkoa wa Shinyanga lakini kwa Mkoa wa Dodoma pekee, watu waliofikiwa ni 683,767, jumla ya Migogoro 543 imepokelewa, Jumla ya migogoro 282 imepata suluhu ya kudumu papo hapo na Mashauri 261 bado yapo katika hatua mbalimbali za utatuzi huku yakifuatiliwa kwa ukaribu na wataalamu wa kisheria
Kampeni hiyo imefanikiwa kuwafikia watu wa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo, makundi maalum, na wananchi wenye migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, ukatili wa kijinsia, pamoja na kutoa Elimu, matunzo ya watoto na kadhalika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)