Justin Wolfers, profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Michigan, katika makala ya New York Times, amekadiria gharama ya vita vya Marekani dhidi ya Iran kuwa trilioni kadhaa za dola.

Katika makala hayo, Justin Wolfers amepinga takwimu iliyotangazwa na Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) kuhusu gharama ya vita dhidi ya Iran, akisema: Takwimu ya dola bilioni 25 iliyotangazwa na Waziri wa Vita wa Marekani, Pete Hegsett inahusiana tu na “uhasibu wa pesa taslimu” wa vifaa vilivyotumika (kama vile makombora 2,000 ya Tomahawk na Patriot). Ameongeza kuwa gharama halisi ni trilioni kadhaa za dola, ambazo Washington inajaribu kuzificha kwa makusudi.

Profesa Justin Wolfers ameonya kwamba iwapo Iran itaimarisha mfumo wa ushuru katika Mlango-Bahari wa Hormuz, mapato yake, (hata yaliwa ya dola moja kwa pipa) yataipa Tehran chanzo kikubwa cha fedha. Hii ina maana kwamba Iran inaweza kutumia pesa inazopata kutokana na kudhibiti biashara ya kimataifa ili kuendeleza miradi ambayo Trump ameapa kuiharibu.

Wakati huo huo, Mikhail Ulyanov, mwakilishi wa Russiia katika mashirika ya kimataifa, ameandika kwenye ukurasa wake binafsi kwenye mtandao wa kijamii wa X, akidhihaki vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Iran na maneno ya uonevu ya kiongozi wa serikali ya kigaidi ya Washington kwamba: “Marekani bado haijaelewa kwamba usaliti na vitisho havifanyi kazi kwa Wairani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *