Jamii imekumbushwa kuibua,Kulea na kukuza vipaji vya watoto ili kuwa na taifa Bora na kupunguza ukosefu wa Ajira

Ni katika msimu wa tatu wa Kiruswa Fun Run ambapo waziri wa habari sanaa utamaduni na Michezo Paul Makonda amesema kuwekeza katika vipaji vya watoto kutawasaidia kuondokana na umasikini na kuchochea Pato la Taifa.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Longido na Naibu waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa na muandaaji wa mbio hizo amesema malengo ya mbio hizo ni kuwaunganisha wana longido, kuimarisha afya na kuibua Vipaji katika michezo mbalimbali.

Nao baadhi ya washiriki hizo wanaeleza mchango wa mbio za hisani katika kukuza mchezo wa riadha nchini.
#StaeTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *