Mwanafunzi wa Shahada ya Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Tukay Thomas, ameibuka mshindi wa shindano la kuwasilisha andiko bunifu lililolenga kupunguza msongamano wa magari mijini kwa kutumia mchanganyiko wa maboresho ya miundombinu, usafiri wa umma na teknolojia za kisasa za usimamizi wa trafiki.
Shindano hilo lililoanzishwa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, lililenga kuibua suluhisho mbadala za kitaalamu kutoka kwa wanafunzi wa uhandisi ili kukabiliana na changamoto sugu ya foleni nchini na kuhamasisha matumizi ya maarifa ya darasani katika vitendo.
Kwa ushindi huo, Tukay amejinyakulia zawadi ya shilingi milioni 10, kompyuta mpakato, tuzo na fursa nyingine za kitaaluma, akiongoza orodha ya washindi katika hafla iliyofanyika Dodoma.
Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo, Waziri Ulega amesema ushindani huo umeonesha ubunifu mkubwa wa vijana na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwashirikisha katika kutatua changamoto za miundombinu na usafiri, ili kuchochea maendeleo endelevu ya taifa.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)