Swali lililoulizwa kwa wanawake kadhaa jijini New York Marekani ni moja tu, Je AI inaweza kuchukua nafasi ya kazi yako? Na jibu la wanawake wote ni Hapana, 

Mama mmoja akaenda mbali zaidi na kusema “sio tu hapana ila ni …. habadani. Kuwa mama au bibi, hii kazi ya ulezi hauwezi kuiondoa” 

© UNICEF/Ian Dobronosov Mama na binti yake wanapita karibu na jengo la viwanda lililoharibiwa kwa kiasi kikubwa mjini Kyiv nchini Ukraine kufuatia shambulio la usiku kucha, huku wazima moto wakiendelea kunyunyiza maji kwenye mabaki ya jengo hilo.

Na kwanini wanawake wanasema hivyo? 

Kuzaa watoto, AI haiwezi kufanya hivyo, AI haiwezi kuwa na hisia zangu ninapo waona watoto wangu wanapoamka na kuniona na kutaka kuwa na mimi na baba yao. 

Mwingine akaeleza jukumu lake la kipekee “Sehemu kubwa ya kazi yangu ni kuwafundisha watoto wangu kuhusu afya ya akili, na nadhani hilo ni jambo ambalo AI haina uwezo wa kuniiga”

Mwanamke mwingine akaeleza yale aliyoyafanya kwa kijana wake kama mzazi “Alivyokwenda chuo kikuu mimi ndio nilikuwa naye bega kwa bega, hakuna AI iliyoweza kumsaidia, ni mama ndio nilifanya kila kitu. 

Pamoja na ukweli huo lakini Akili Mnemba AI inasaidia kufanya mengi, na bibi huyu anatoa wito kwa wanawake wengine wa makamo. “Watu wa umri wangu wamekuwa na uwoga, lakini nadhani AI inaweza kunisaidia katika maeneo ambayo nitafika na sitakuwa na uwezo wa kufanya vitu na wajukuu zangu.”

Mwingine anasema “Mimi ni mama ninayefanya kazi, muda kidogo nilionao ninapokuwa na watoto wangu ni muda wa kipekee sana kwangu.” 

Je wewe AI inaweza kuchukua ajira yako? 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *